Connect with us

Ahmad:Hatujaamua kuwa Ivory Coast haitakuwa mwenyeji wa AFCON 2021

Ahmad:Hatujaamua kuwa Ivory Coast haitakuwa mwenyeji wa AFCON 2021

Ahmad: Hatujaamua kuwa Ivory Coast haitakuwa mwenyeji wa AFCON 2021

 Na Victor Abuso,

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limesema halijafikia uamuzi wowote wa kuipa nafasi nchi ya Ivory Coast kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la Afrika mwaka 2023 badala ta 2021.

Kauli hii ya CAF imekuja, baada ya rais wa Shirikisho hilo Ahmad Ahmad kunukuliwa akisema kuwa Cameroon imepewa nafasi ya kuwa mwenyeji mwaka 2021.

Ahmad amesema kuwa, alinukuliwa vibaya.

Camerron iliondolewa uwenyeji wa kuandaa fainali za mwaka 2019, kwa sababu ya maandalizi mabaya lakini pia suala la usalama.

Ivory Coast imekwenda katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo, kupinga uwezekano wowote wa kupokonywa haki za kuandaa fainaliza mwaka 2021.

Wakati uo huo, mwenyeji wa AFCON mwaka 2019, anatarajiwa kutajwa tarehe 9 mwezi Januari 2019.

Misri na Afrika Kusini zimethibitisha kuwa mwenyeji wa fainali hiyo itakayofanyika kayi ya mwezi Juni na Julai na kwa mara ya kwanza, mataifa 24 yanatarajiwa kushiriki.

Chiyangwa, kuendelea kuongoza COSAFA

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Zimbabwe Philip Chiyangwa, atasalia kuongoza Shirikisho la mchezo huo katika nchi za Kusini mwa bara la Afrika COSAFA.

Uamuzi huu, umechukuliwa na uongozi wa COSAFA kwa sababu sheria haimzuii kushikilia nafasi hiyo, licha ya kutokuwa rais wa soka nchini mwake.

Chiyangwa ambaye alizolea umaarufu barani Afrika, baada ya kusaidia kuchaguliwa kwa rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad, alishindwa wakati wa Uchaguzi wa urais wa Shirikisho la soka nchini humo jijini Harare, Jumapili iliyopita.

Rais mpya wa soka nchini Zimbabwe ni Felton Kamambo.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in