Connect with us

Shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA) limekubali kuvunja mkataba wa kocha wa timu ya taifa Mjerumani Antoine Hey.

Hey amewaomba viongozi wa soka nchini Rwanda wamruhusu aondoke baada ya matokeo mabaya katika michuano ya CHAN kutafuta ubingwa wa bara Afrika kwa wachezaji wanaocheza katika ligi za nyumbani.

Amavubi Stars waliondolewa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco. Haikufungana na Nigeria, ikaifunga Equatorial Guinea bao 1-0 na kupoteza mchuano wake wa mwisho dhidi ya Libya kwa kulazwa bao 1-0.

Kocha Hey anaondoka Rwanda, licha ya kusalia na miezi miwili katika mkataba aliotia saini na viongozi wa soka nchini Rwanda mwezi Machi mwaka 2017.

Rais wa FERWAFA Vincent Nzamwita amesema pamoja na kwamba wamekubali ombi la Hey, itabidi atekeleze matakwa ya mkataba huo kwa uamuzi wake wa kuondoka mapema.

Ripoti zinasema kuwa, huenda Hey akaenda kuifunza timu ya taifa ya Syria baada ya kuondoka Rwanda.

Amewahi pia kuifunza Kenya, Lesotho na Gambia.

More in African Football