Connect with us

AFCON 2017: Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yaandikisha matokeo tofauti

AFCON 2017: Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yaandikisha matokeo tofauti

Na Victor Abuso,

Timu za taifa ya soka za Afrika Mashariki na Mashariki na Kati ziliaza michuano ya kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 kwa kupata matokeo mbalimbali.

Uganda Cranes wakiwa nyumbani, katika uwanja wa Kimataifa wa Naambole jijini Kampala walipata ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Bostwana.

Vijana wa kocha Milutin Micho walipata mabao yao kupitia nahodha Geofrey Massa na Umony Brian.

Ushindi huo umeendelea kuonesha rekodi ya Uganda kutofungwa nyumbani kwa kipindi kirefu na wamejipatia alama tatu muhimu sawa na Burkina Faso ambao pia waliwafunga Comoros mabao 2 kwa 0.

Mwezi Septemba, Uganda watakuwa ugenini kumenyana na Comoros huku Burkina Faso wakicheza na Bostwana katika kundi hilo.

Tanzania ikiwa mjini Alexandria nchini Misri, walifungwa mabao 3 kwa 0 katika mchuano wao wa kwanza wakiwa ugenini.

Mabao ya Pharaohs yalitiwa kimyani na Rami Rabia, Bassem Morsy huku Mohamed Salha akifunga la tatu na kuihakikishia timu yake ushindi.

Misri sasa itasafiri Chad mwezi Septemba, lakini Tanzania watakuwa nyumbani kuwakaribisha Super Egales ya Nigeria.

Kwa matokeo haya, Misri wana alama tatu sawa na Nigeria ambao waliwafunga Chad mabao 2 kwa 0.

Tanzania na Chad hawana alama yoyote.

Amavubi Stars ya Rwanda ilianza vizuri kwa kupata ushindi ugenini kwa kuifunga Msumbiji bao 1 kwa 0 katika uwanja wa Estadio Nacional Do Zimpeto mjini Maputo.

Bao la ushindi la Rwanda lilitiwa kimyani na Ernest Sugira katika dakika ya tatu ya mchuano huo kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Jacques Tuyisenge.


Mambas ya Msumbiji wakiwa nyumbani walitawala mchezo huo na kuishambulia ngome ya Rwanda lakini ikashindwa kupenya katika ngome ya ulinzi.

Kocha Johnny McKinstry sasa inajiandaa kuchuana na Black Stars ya Ghana mwezi Septemba na kwa ushindi wa mwishoni mwa juma lililopita, ina alama tatu sawa na Ghana ambayo iliishinda Mauritus mabao 7 kwa 1.


Harambee Stars ya Kenya nayo ikiwa jijini Brazzaville ililazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Congo.

Kenya ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji Paul Were.

Hata hivyo, dakika chache kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza mchezaji wa Kenya Jackson Saleh aliunawa mpira na kuwapa Congo nafasi ya kupewa penalti waliofunga .

Kwa matokeo haya, Kenya na Congo zina alama moja sawa na Zambia na Guinea Bissau ambao walitoka sare ya kutofungana mwishni mwa juma lililopita.

Mwezi Septemba, Kenya watakuwa nyumbani kucheza na Zambia huku Congo wakimenyana na Guinea Bissau.

Intamba Murugamba ya Burundi ilianza vibaya kwa kupoteza baada ya kufungwa na Senegal mabao 3 kwa 1 jijini Dakar huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikijipatia alama tatu muhimu kwa kuwafunga Madagascar kwa mabao 2 kwa 1.

Ethiopia pia ilianza vema kwa kujipatia alama tatu muhimu baada ya kutoka nyuma na kuwafunga Lesotho mabao 2 kwa 1.

Sudan ikiwa nyumbani ilianza kwa kupata ushindi wa bao 1 kwa 0 baada ya kuwafunga Sierra Leone.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in