Connect with us

AFCON 2017: McKinstry ataja kikosi cha kuishinda Mauritius

AFCON 2017: McKinstry ataja kikosi cha kuishinda Mauritius

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Rwanda Johnathan McKinstry, amekitaja kikosi cha wachezaji 26 kumenyana na Mauritius katika mchuano muhimu wa kundi H kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017.

Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa Anjalay mjini Belle-Vue, tarehe 26 na baadaye mchuano wa marudiano tarehe 29 katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali.

Rwanda inakwenda katika mchuano hii ikiwa ya pili kwa alama 3 katika kundi hilo, baada ya kupata ushindi katika mchuano wao dhidi ya Msumbiji wa bao 1 kwa 0 mwaka uliopita na baadaye kufungwa na Ghana bao 1 kwa 0.
Kundi hili linaongozwa na Ghana ambayo ina alama 6.

Kocha McKinstry, amewateua wachezaji sita katika kikosi  chake cha mwisho pamoja na 20 wanaocheza soka nyumbani.

McKinstry amesema ni lazima vijana wake, washinde ugenini na nyumbani ili kuendelea kuweka hai matumaini  yao ya kufuzu katika fainali ya mwaka 2017 nchini Gabon.

Wachezaji walioitwa watakutana siku ya Jumamosi jijini Kigali na kuanza mazoezi ya pamoja kabla ya kuondoka nchini humo siku ya Alhamisi juma lijalo kwenda nchini Mauritius.

Kikosi kamili

Makipa: Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Olivier Kwizera (APR Fc), Marcel Nzarora (Police Fc) and Andre Mazimpaka (Mukura VS)

Mabeki: Michel Rusheshangoga (APR Fc), Fitina Omborenga (SC Kiyovu), Celestin Ndayishimiye (Mukura VS), Abouba Sibomana (Gor Mahia, Kenya), Soter Kayumba (AS Kigali), Abdul Rwatubyaye (APR Fc), Emery Bayisenge (APR Fc) and Salomon Nirisarike (STVV)

Viungo wa Kati: Yannick Mukunzi (APR Fc), Djihad Bizimana (APR Fc), Jean Baptiste Mugiraneza (Azam Fc, Tanzania), Amran Nshimiyimana (Police Fc), Haruna Niyonzima (Young Africans, Tanzania), Dominique Savio Nshuti (Rayon Sports), Innocent Habyarimana (Police Fc), Jean Claude Iranzi (APR Fc), Yussufu Habimana (Mukura VS) and Muhadjiri Hakizimana (Mukura VS)

Washambuliaji:Ernest Sugira (AS Kigali), Quentin Kwame Rushenguziminega (Laussane Sport, Swiss), Elias Uzamukunda (Le Mans, France) and Dany Usengimana (Police Fc).

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in