Connect with us

Fahamu kwa kina uchambuzi wa michuano ya kundi D kuelekea michuano ya ufunguzi siku ya Jumamosi nchini Gabon.

Ghana

Hii ni fainali ya 21 ya Black Stars ya Ghana.

Mara ya mwisho kushiriki katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2015.

Mara ya mwisho kushinda taji hili ilikuwa ni mwaka 1982. Lakini pia imewahi kushinda taji hili mwaka 1963,1965 na 1978.

Mwaka 2015, Ghana ilifika katika hatua ya fainali lakini ikashindwa mbele ya Ivory Coast kwa penalti 9-8 baada ya mchuano huo kumalizika kwa sare ya kutofungana.

Safari ya kwenda Gabon

Ghana ilifuzu katika fainali hii baada ya kushinda mataifa mengine ya Msumbiji, Rwanda na Mauritius.

Kati ya mechi sita ilizocheza, Ghana ilishinda mechi nne, ikatoka sare michuano miwili na hivyo kumaliza kundi hilo kwa ushindi wa alama 14.

Kocha

Mkufunzi wa Black Stars ni Avram Grant raia wa Israeli. Ajipewa kibarua cha kuifunza, Ghana mwaka 2014 baada ya kuchukua nafasi ya Kwesi Appiah.

Grant mwenye umri wa miaka 61, ni miongoni mwa makocha wachache barani Afrika ambao wana uzoefu mkubwa wa kufunza soka.

Kabla ya kuifunza Ghana, aliwahi pia kuifunza nchi yake ya Israel kati ya mwaka 2002-2006.

Mbali na timu za taifa, amewahi pia kufunza vlabu vya Portsmouth, West Ham United na Chelsea ya Uingereza.

Kikosi:

Kocha Grant amekitaja kikosi chake cha mwisho kuelekea nchini Gabon.

Makipa: Razak Braimah (Cordoba, Uhispania), Abdul-Fatau Dauda (Enyimba, Nigeria), Richard Ofori (Wa All Stars)

Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, Marekani), Andy Yiadom (Barnsley, Uingereza), Baba Rahman (Schalke, Ujerumani), Frank Acheampong (Anderlecht, Ubelgiji), (John Boye (Sivasspor, Uturuki), Jonathan Mensah (Columbus Crew, Marekani), Daniel Amartey (Leicester City, Uingereza), Edwin Gyimah (Orlando Pirates, Afrika Kusini)

Viungo wa Kati: Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italia), Afriyie Acquah (Torino, Italia), Thomas Partey (Atletico Madrid, Uhispania)  Mubarak Wakaso (Panathinaikos, Ugiriki), Christian Atsu (Newcastle, Uingereza), Ebenezer Ofori (AIK Stockholm, Sweden), Samuel Tetteh (Leifering, Austria)

Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ahly, Falme za Kiarabu) Jordan Ayew (Aston Villa, Uingereza), Andre Ayew (West Ham, Uingereza), Ebenezer Assifuah (Sion, Switzerland), Bernard Tekpetey (Schalke, Ujerumani)

Maandalizi

Ghana imekuwa katika maandalizi ya michuano hii mjini Dubai katika nchi ya Falme za kiarabu.

Kikosi hiki kinatarajiwa kuwasili nchini Gabon tarehe 15.

Black Stars, imejumuishwa katika kundi moja na Mali, Misri na Uganda.

Mchuano wa kwanza utakuwa dhidi ya Uganda tarehe 17 dhidi ya Uganda mjini Port-Gentil.

Mali

Mali inashiriki katika makala ya 10 ya michuano hii. Inafahamika kwa jina maarufu la Les Aigles (The Eagles).

Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2015 Equitorial Guinea, lakini ikaondolewa katika hatua ya makundi.

Haijawahi kushinda taji hili lakini mwaka 1972, ilimaliza katika nafasi ya pili katika michuano hiyo.

Safari ya kwenda Gabon.

Mali ilifuzu katika michuano hii baada ya kuongoza kundi la C, kufuzu kwenda nchini Gabon baada ya kumaliza ya kwanza kwa alama 16, mbele ya Benin, Equitorial Guinea na Sudan Kusini.

Kati ya mchezi sita ilizocheza, The Eagles walifanikiwa kupata ushindi katika michuano mitano na kutoka sare mchuano mmoja.

Kocha

Kocha wa Mali ni Mfaransa, Alain Giresse.

Giresse mwenye umri wa miaka 64, aliugana na Mali mwaka 2015, lakini amewahi kuifunza nchi hiyo kati ya mwaka 2010-2012.

Gabon ilikuwa nchi yake ya kwanza kufunza barani Afrika kati ya mwaka 2006-2010 na Senegal kati ya mwaka 2013-2015.

Mbali na timu za taifa, amewahi pia kufunza FAR Rabat ya Moroco kati ya mwaka 2001-2003, Tolouse na Paris Saint-Germain nchini Ufaransa lakini pia kati ya mwaka 2004-2005, aliifunza timu ya taifa ya Georgia.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Bordeaux na Marseille lakini pia timu ya taifa ya Ufaransa.

Kikosi

Makipa: Soumaila Diakité and Djigui Diarra (Stade Malien de Bamako), Oumar Sissoko (Orléans, Ufaransa)

Defenders: Ousmane Coulibaly (Panathinaikos, Ugiriki), Hamari Traore (Reims, Ufaransa), Molla Wagué (Udinese, Italia), Salif Coulibaly (TP Mazembe, DR Congo), Mohamed Oumar Konaté (RS Berkane, Morocco), Mahamadou N’Diaye (Troyes, Ufaransa), Youssouf Koné (Lille, Ufaransa)

Midfielders: Yves Bissouma (Lille, Ufaransa), Mamoutou N’Diaye (Royal Antwerp, Ubelgiji), Lassana Coulibaly (Bastia, Ufaransa), Yacouba Sylla (Montpellier, Ufaransa), Samba Sow (Kayserispor, Uturuki), Adama Traoré (AS Monaco, Ufaransa), Sambou Yatabaré (Werder Bremen, Ujerumani)

Forwards: Moussa Marega (Vitória Guimarães, Ureno), Kalifa Coulibaly (Gent, Ubelgiji), Moustapha Yatabaré (Karabukspor, Uturuki), Bakary Sako (Crystal Palace, Uingereza), Moussa Doumbia (Rostov, Urusi).

Maandalizi

Mali inapiga kambi mjini Casablanca Morocco kabla ya kwenda nchini Gabon.

Imepangwa katika kundi moja na Uganda, Misri na Ghana.

Uganda

Uganda Cranes inarejea katika fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978.

Haya ni mashindano ya 6 kwa Uganda ambayo mara ya wkanza ilishiriki mwaka 1962 na kumaliza wa nne.

Historia ya mwaka 1978 bado inakumbukwa kwa sababu, Uganda ilifika katika hatua ya fainali na Ghana lakini kwa bahati mbaya haikufanikiwa kushinda taji hilo.

Safari ya kwenda Gabon

Uganda ilikuwa katika kundi moja na Burkina Faso, Botswana na Comoros kutafuta nafasi ya kwenda nchini Gabon.

Kati ya mechi sita ilizocheza nyumbani na ugenini, ilishinda mechi nne, ikatoka sare mchuano mmoja na kufungwa mmoja.

Ilimaliza kundi hilo katika nafasi ya pili kwa alama 13, nyuma ya Burkina Faso ambayo pia ilikuwa na alama 13 lakini wingi wa mabao.

Uganda Cranes ilifuzu kama mshindi wa pili wa michuano hiyo ya kufuzu.

Kufuzu kwa Uganda kulileta furaha kubwa sana nchini humo lakini pia katika nchi jirani za Afrika Mashariki, baada ya miaka 38, ya kutafuta tiketi hiyo.

Kocha

Kocha wa Uganda ni Mserbia, Milutin Sredojević maarufu kama Micho.

Micho mwenye umri wa miaka 47, alianza kuifunza Uganda Cranes kuanzia mwaka 2013, baada ya kuchukua nafasi iliyoachwa na Bobby Williamson kutoka Scotaland.

Ameisaidiwa Uganda kushinda taji la kila mwaka la timu bora mwaka 2016, baada ya kuisaidia kufuzu michuano ya AFCON 2017.

Mbali na Uganda, Micho aliwahi kuifunza Rwanda kati ya mwaka 2011-2013.

Ametajwa kuwa miongoni mwa makocha waliofunza soka barani Afrika kwa muda mrefu.

Amewahi kuifunza Sports Club Villa ya Uganda, Saint-George ya Ethiopia, Orlando Pirates, Yanga FC ya Tanzania, Al-Hilal Omdurman ya Sudan.

Kikosi

Makipa: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/Afrika Kusini) , Robert Odongkara (Saint George/Ethiopia) Salim Jamal (AL Merreikh/Sudan)

Mabeki: Joseph Ochaya (KCCA) Timothy Dennis Awany (KCCA) Shafik Batambuze (Tusker/KEN) Dennis Iguma (Al Ahed/Lebanon ) Isaac Isinde (Hana klabu) Murushid Juuko (Simba/Tanzania) Nicholas Wadada (Vipers)

Viungo wa Kati: Tony Mawejje (Throttur/Iceland) Khalid Aucho (Baroka/Afrika Kusini) Luwagga William Kizito (Rio Ave/Ureno) Moses Oloya (Hanoi T and T/VIE) Geoffrey Kizito (Than Quang Ninh/Vietnam) Godfrey Walusimbi (Gor Mahia/Kenya) Hassan Mawanda Wasswa (Nijmeh/Lebanon) Mike Azira (Colorado Rapids/Marekani)

Washambuliaji: Faruku Miya (Standard Liege/Ubelgiji) Geoffrey Massa (Baroka/Afrika Kusini) Muhammad Shaban (Onduparaka) Yunus Sentamu (Ilves/Finland), Geoffrey Sserunkuma (KCCA).

Maandalizi

Uganda inapiga kambi mjini Dubai katika Mmiliki za kiarabu. Mchuano wa kirafiki dhidi ya Tunisia na Ivory Coast.

Imepangwa pamoja na Ghana, Misri na Togo.

Misri

Haya yatakuwa mashindano ya 23 kwa timu ya taifa ya Misri.

Misri inayofahamika kama Pharaohs, wanarejea katika michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara ya mwisho mwaka 2010.

Inasalia kuwa taifa bora, kuweka historia ya kushinda mataji mengi ya taji hili, mara 7 mwaka 1957,1959,1986,1998,2006,2008 na 2010.

Safari ya kwenda Gabon

Misri ilipangwa katika kundi moja na Nigeria na Tanzania katika michuano ya kufuzu kwa fainali ya mwaka huu.

Kati ya mechi nne ilizocheza nyumbani na ugenini baada ya Chad kuondolewa katika michuano hiyo, ilishinda mechi tatu na kutoka sare mchuano mwingine na hivyo kuongoza kundi la G kwa alama 10.

Hali ya kisiasa imekuwa ikielezwa kuwa moja ya sababu ya Misri kukosa kufika katika michuano hii tangu mwaka 2010, na kuwepo kwao huenda kukaleta ladha tofauti.

Kocha.

Kocha wa timu hii ni raia wa Argetina Héctor Cúper.

Cúper mwenye umri wa miaka 61, alianza kuifunza Misri mwaka 2015.

Misri ndio timu ya kwanza ya taifa kufunzwa na kocha huyu ambaye ana uzoefu mkubwa kufuza soka katika vlabu mbalimbali.

Alianza kufunza soka mwaka 1993, wakati huo akiifunza klabu ya Huracan.

Aidha, amewahi kuifunza Internationale ya Italia kati ya mwaka 2001-2003, Mallorca 2004-2006 na Parma mwaka 2008.

Kabla ya kupewa kibarua nchini Misri, alikuwa anaifunza Al Wasl FC kutoka Falme za Kiarabu kati ya mwaka 2013-2014.

Kikosi

Makipa: Ahmed El-Shennawy (Zamalek), Essam El-Hadary (Wadi Degla), Sherif Ekramy (Al Ahly)  

Mabeki: Ahmed Fathi (Al Ahly), Ahmed Elmohamady (Hull City – Uingereza), Mohamed Abdel-Shafy (Al-Ahli – Ksa), Karim Hafez (Lens – Ufaransa), Ahmed Hegazy (Al Ahly), Saad Samir (Al Ahly), Ahmed Dweidar (Zamalek), Ali Gabr (Zamalek), Omar Gaber (Basel – Uswizi).

Viungo wa Kati: Mohamed Elneny (Arsenal – Uingereza), Tarek Hamed (Zamalek), Ibrahim Salah (Zamalek), Abdallah El-Said (Al Ahly), Amr Warda (Panetolikos – Ugiriki), Ramadan Sobhi (Stoke City – Uingereza), Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ (Royal Mouscron – Ubelgiji).  

Washambuliaji: Ahmed Hassan ‘Koka’ (Braga – Ureno), Marwan Mohsen (Al Ahly), Mahmoud Abdel-Moneim ‘Kahraba’ (Al-Ittihad – Ksa), Mohamed Salah (As Roma – Italia).

Maandalizi

Misri ambayo ipo katika kundi D na Ghana, Mali na Ghana. Itacheza michezo yake ya makundi katika mji wa Port Gentil.

Misri ambao wamekuwa wakifanya mazoezi yao mjini Cairo, watamenyana na Mali katika mchuano wao wa ufunguzi tarehe 17.

More in