Connect with us

 

Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya DR Congo skipper Youssouff Mulumbu anasema amesikitika kuvuja kwa mkanda wa video unaowaonesha wachezaji wakilalamikia kulipwa marupurupu yao na kususia mazoezi nchini Gabon.

Mulumbu amesema kuwa malalamishi yao yameshashughulikiwa ipasavyo na wachezaji wako tayari kumenyana na Morocco katika mchuano wake wa kwanza siku ya Jumapili.

Mulumba anayecheza soka katika klabu ya Norwich City nchini Uingereza, alionekana katika mkanda huo akiiambia serikali ya DRC kutimiza ahadi ya kuwalipa marupurupu yao la sivyo hawatafanya mazoezi.

Baada ya kuonekana kwa mkanda huo, serikali ya DRC ilituma ujumbe wa maafisa 100 wakiongozwa na Waziri wa Michezo Willy Bakonga walikwenda nchini Gabon kuzungumza na wachezaji hao.

DR Congo walioshinda taji hili mara mbili mwaka 1968 na 1974, watashuka kumenyana na Morocco katika uwanja wa Oyem kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Hata hivyo, mchuano wa ufunguzi wa kundi C, mabingwa watetezi Ivory Coast watamenyana na Togo kuanzia saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.

Ratiba ya Jumanne kundi D

Ghana vs Uganda

Mali vs Misri

Matokeo yaliyopita:

Kundi A:- Gabon 1-1 Guinea-Bissau

Burkina Faso 1-1 Cameroon

Kundi B:-Algeria 2-2 Zimbabwe

Tunisia 0-2 Senegal

More in