Connect with us

 

Mechi za mchezo wa soka mzunguko wa pili hatua ya makundi kutafuta ubingwa wa bara Afrika, zinaanza kuchezwa siku ya Jumatano nchini Gabon.

Wenyeji Gabon wanarejea tena katika uwanja wa Amitie, jijini Libreville kumenyana na Burkina Faso.

Mechi hii itachezwa kuanzia saa moja kamili jioni saa za Afrika Mashariki, chini ya refarii kutoka Gambia Bakary Gasssama.

Gabon inatumai kuwa itaandikisha ushindi leo, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika mzunguko wa pili na kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani.

Baadaye, Cameroon itachuana na Guinea-Bissau inayoshiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza.

Uchambuzi wa kina

Hadi sasa, ni mataifa matatu kati ya 16 yanayoshiriki katika michuano hii ambayo yamepata ushindi katika mzunguko wa kwanza.

Mataifa yaliyopata ushindi ni pamoja na Senegal iliyoifunga Tunisia mabao 2-0 na sasa inaongoza kundi la B kwa alama tatu, mbele ya Algeria, Zimbabwe na Tunisia.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nayo ilianza vema baada ya kuishinda Morocco kwa bao 1-0.

Leopard ndio timu pekee iliyopata ushindi katika kundi la C.

Ghana pia ni timu nyingine, ambayo imefanikiwa kupata ushindi katika mzunguko wa kwanza.

Siku ya Jumanne usiku, iliishinda Uganda bao 1-0 mjini Port-Gentil katika mchuano wa kundi D.

Matokeo ya sare katika makundi yote.

Kundi A

Gabon 1-1 Guinea-Bissau

Burkina Faso 1-1 Cameroon

Kundi B

Algeria 2-2 Zimbabwe

Kundi C

Ivory Coast 0-0 Togo

Kundi D

Mali 0-0 Misri

Wachambuzi wa soka wanasema sare hii inamaanisha kuwa kuna ushindani mkali sana katika makala haya 31 ya AFCON.

More in