Connect with us

AFCON 2017:Micho ataja kikosi cha wachezaji 24

AFCON 2017:Micho ataja kikosi cha wachezaji 24

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uganda Milutin Sredojevic amekitaja kikosi cha wachezaji 24 kwa maandalizi ya mchuano dhidi ya Comoros kufuzu latika fainali za ubingwa wa Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Kikosi hicho kina makipa 4, mabeki 8, viungo wa kati 8 na washambuliaji 4.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza mazoezi siku ya Jumatatu tarehe 31 mwezi huu wa Agosti.

Micho amesema kuwa kikosi cha mwisho kitakuwa na makipa wawili, mabeki sita, viungo wa kati saba na washambuliaji watatu.

Uganda ambayo ipo katika kundi moja na Burkina Faso na Bostwana na itamenyana na Comoros ugenini mapema mwezi ujao.

Cranes walianza vizuri kampeni za kwenda Gabon kwa ushindi wa mabai 2 kwa 0 dhidi ya Bostwana mwezi Juni katika mchuano wao kwanza wa makundi na ina alama tatu sawa na Burkina Faso.

Kikosi Kamil

Makipa:

Dennis Onyango (Mamelodi Sun Downs, Afrika Kusini), Ismail Watenga (Vipers, Uganda), Robert Odongkara (St George, Ethiopia), Salim Jamal (El Merriekh, Sudan)

Mabeki:

Denis Iguma (Al Ahed, Lebanon), Joseph Ochaya (KCCA, Uganda), Murushid Juuko (Simba, Tanzania), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya), Denis Okot (KCCA, Uganda), Shafik Bakaki (Vipers, Uganda), Richard Kasagga Jjuuko (URA, Uganda), Isaac Isinde (St George)

Viungo wa Kati:

Yasser Mugerwa (Orlando Pirates, Afrika Kusini), Aucho Khalid (Gor Mahia, Kenya), Farouk Miya (Vipers, Uganda), William Luwagga Kizito (Rio Avio, Portugal), Muzamiru Mutyaba (KCCA, Uganda), Kizironi Kizito (Vipers, Uganda), Tonny Mawejje (Thróttur Reykjavík, Iceland), Ivan Ntege (KCCA, Uganda)

Washambuliaji:

Geofrey Massa (Bloemfontein Celtics, Afrika Kusini), Brian Umony (St George, Ethiopia), Yunus Sentamu (Club Sportif Sfaxien, Tunisia), Robert Sentongo (URA, Uganda)

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in