Connect with us

Africa Cup of Nations

AFCON 2019: Kenya na Tanzania, nani ataibuka mbabe ?

AFCON 2019: Kenya na Tanzania, nani ataibuka mbabe ?

Timu za taifa za Kenya na Tanzania zitachuana Alhamisi usiku katika mechi muhimu ya mchezo wa soka, kuwania taji la bara Afrika, michuano inayoendelea nchini Misri.

Mataifa haya mawili yapo katika kundi C na mechi hiyo itachezwa kuanzia saa tano usiku saa za Afrika Mashariki katika wa uwanja wa June 30 jijini Cairo.

Harambee Stars inakwenda katika mechi hii ya pili baada ya kuanza vibaya, kwa kufungwa na Algeria mabao 2-0 sawa na Taifa Stars ambayo ilifungwa na Senegal pia mabao 2-0.

Hii ni mara ya kwanza kwa mataifa ya Afrika Mashariki kutoka ukanda wa CECAFA ndani ya miaka 43 kucheza katika michuano hii mikubwa barani Afrika.

Kuelekea katika mchuano huu mkubwa kati ya majirani hawa wawili, mashabiki wa kila upande wanaamini kuwa, timu yao itafanya vema katika mchuano huo ambao kila timu inahitaji kushinda ili kuwa na matumaini ya kufuzu katika hatua ya 16 bora.

Historia kati ya nchi hizi mbili inaonesha kuwa, zimekutana mara 44. Kenya imeshinda mara 20, ikatoka sare mara 14 huku Tanzania ikishinda mara 14.

Ratiba ya Alhamisi, Juni 29 2019

Madagascar vs. Burundi
Senegal vs. Algeria
Kenya vs. Tanzania

Michuano nyingine ya AFCON kati ya nchi za Afrika Mashariki

Januari 12, 1968: 
Ethiopia 2-1 Uganda

Februari 6, 1970: 
Sudan 3-0 Ethiopia

Februari 29, 1976: 
Ethiopia 2-0 Uganda

More in Africa Cup of Nations