Connect with us

Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Ghana, itacheza mechi yake ya pili dhidi ya Cameroon kutafuta ushindi wa pili, katika fainali ya kuwania taji la wanawake barani Afrika.

Fainali hii ilianza wiki iliyopita jijini Accra.

Wenyeji walianza vema baada ya kuishinda Algeria bao 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Cameroon nao walianza kwa ushindi baada ya mechi yake ya kwanza kwa kuishinda Mali mabao 2-1.

Mechi nyingine hivi leo ni kati ya Mali na Algeria.

Kesho, Nigeria itamenyana na Zambia. Equitorial Guinea itachuana na Afrika Kusini.

 

 

More in AWCON