Connect with us

Klabu ya Azamimeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kumsajili beki wa kimataifa wa Uganda, Nicholaus Wadada.

Wadada mlinzi wa pembeni amesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Vipers ya Uganda.

Kabla ya kusajiliwa na Azam , Wadada pia alikuwa akitajwa kuwaniwa na Simba na Yanga.

Anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Kocha mpya wa Azam, Hans Pluijm. Wengine waliosajiliwa ni Tafadzwa Kutinyu, Donald Ngoma na Ditramu Nchimbi.

Aidha klabu hiyo imefanikiwa kumrejesha kundi mchezaji Mudathir Yahya ambaye msimu uliopita aliitumikia Singida United.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in