Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Beki wa kimataifa wa Tanzania Abdi Banda amesema ataitumia vyema Ligi ya Afrika Kusini ili afanikiwe kucheza soka barani Ulaya.

Mchezaji huyo alijiunga na Baroka FC katika kipindi hiki cha usajili kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na miamba ya Tanzania, Simba SC

Banda alianza kuitumikia timu yake katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Afrika Kusini dhidi ya Polokwane City, mechi iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana.

“Nilipenda sana kucheza Afrika Kusini na nimefanikiwa, naitumia hii kama changamoto ili nifike mbali,”alisema.

Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Baroka FC.

More in