Connect with us

Brazil ndio mabingwa wa mchezo wa soka kwa vijana, katika mashindano ya Olimpiki ambayo yamemalizika nchini Argentina.

Vijana wa Brazil walinyakua medali ya dhahabu kwa kuifunga Urusi mabao 4-1.

Wachezaji wa Misri nao walifanikiwa, kunyakua medali ya shaba, baada ya kumaliza wa tatu.

Katika mechi ngumu, vijana kutoka Misri waliwashinda wenyeji Argentina mabao 5-4.

Mataifa 10 yaliyoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Brazil, Urusi, Misri, Argentina, Iraq, Iran, Slovakia, Costa Rica, Panama na Solomon Islands

More in Swahili Stories