Connect with us

By Fadhili Sizya,

Timu ya taifa ya Burundi chini ya miaka 23  imefanikiwa kuvuka mzunguko wa pili baada ya kuishinda Tanzania  chini ya miaka hiyo kwa sheria ya bao la ugenini licha ya kufungwa 3-1 katika mechi hizo za vijana kufuzu Afcon mwaka 2019.

Mechi hiyo ya mkondo wa pili ilichezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam majira ya saa 07:00 usiku ilikuwa mchuano mkali baada ya mechi ya awali iliyochezwa Bujumbura uwanjani Prince Louis Rwagasore kumalizika kwa vijana hao wa Burundi kuibuka na ushindi wa 2-0.

Vijana wa Tanzania walitangulia kwa bao la Habib Kyombo dakika ya 4 kisha Mbaraka Yussuf akafunga la pili dakika ya 43 na kupelekea vijana hao kwenda mapumziko wakiongoza 2-0.

Kipindi cha pili vijana hao wakafanikiwa kuongeza bao la 3 kupitia kwa Salum Kihimbwa aliyepiga shuti kali baa ya kipa wa Burundi kuutema mpira wa krosi dakika ya 70, wakati wakiwa na furaha hiyo wakajisahau kuimarisha ulinzi na mnamo dakika ya 89 kijana Cedric Mavugo akafunga bao la kufutia machozi kwa Burundi na ikawa tiketi ya kuvuka hatua hiyo kwa sheria ya bao la ugenini.

Afcon U23 hufanyika kila baada ya miaka minne na uzito wake hujumuisha na mechi za kufuzu Olimpic na jumla ta timu nane zitacheza katika mechi za mwisho za mashindano hayo.

Afcon U23 2019 itakuwa ni mara ya tatu kufanyika, ambapo nchi ya Misri watakuwa wenyeji kuanzia Novemba 8-22 mwaka ujao.

 

 

More in