Connect with us

CAF: AS Vita Club yaondolewa katika michuano ya Shirikisho

CAF: AS Vita Club yaondolewa katika michuano ya Shirikisho

 Na Victor Abuso,

Klabu ya Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeondolewa nje ya michuano ya Shirikisho barani Afrika licha ya kupata ushindi wa mabao 3 kwa 2  dhidi ya Stade Malien katika mechi ya mwondoano mwishoni mwa juma lililopita.

Mchuano huo ulichezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Tata Raphael jijini Kinshasa.

Stade Malien ilifuzu baada ya kupata ushindi katika mchuano wa mzunguko wa kwanza kwa kuwashinda AS Vita Club mabao 2 kwa 0 jijini Bamako.

Vita club walistahili kupata ushindi wa mabao 3 bila ya kufungwa kuwa na uhakika wa kusonga mbele,  lakini vijana wa kocha  Florent Ibengé walishindwa kulifanikisha hilo.

Msimu uliopita, AS Vita Club ilifika katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Katika matokeo mengine, Orlando Pirates ya Afrika Kusini imefuzu kwa jumla ya mabao 6 kwa 1 baada ya kuishinda Kaloum Star ya Guinea.

Etoile du Sahel ya Tunisia licha ya kupoteza mchuano wa kwanza dhidi ya Raja Casablanca ya Morroco.

CS Sfaxien ya Tunisia pia imefuzu baada ya kuishinda ASEC ya Cote Dvoire.

Sanga Balende ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikaoondolewa na Zamalek ya Misri.

Vlabu vingine vilivyofuzu katika hatua ya robo fainali ni pamoja na ES Tunis ya Tunisia, Al Ahly ya Misri na AC Leopard ya Congo Brazaville.

Michuano ya robo fainali nyumbani ya ugenini zimeratibiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu, na Esperance de Tunis, Etoile du Sahel zote za Tunisia, Al-Ahly ya Misri na Stade Malien ya Mali zimejumuishwa katika kundi moja.

Kundi lingine ni pamoja na Zamalek ya Misri, CS Sfaxien ya Tunisia, AC Leopards ya Congo na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.


Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in