Connect with us

Klabu ya Gor Mahia ilipata bao la dakika za lala salama, kuishinda Nyasa Big Bullets ya Malawi bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.

Bernard Ondiek, aliingia uwanjani, na kuisaidia klabu kupata ushindi huo muhimu, katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Michezo wa Kasarani siku ya Jumatano

Ilikuwa ni mechi ya kwanz ana muhimu kwa kaimu koch Zedekiah Otieno ambaye, alimwanzisha mchezaji mpya Erisa Ssekisambua kutika Uganda, akishirikiana na Jacques Tuyisenge pamoja na Kenneth Muguna.

Mechi ya marudiano, itachezwa baada ya wiki moja jijini Blantyre, wiki ijayo.

Matokeo mengine ya mzunguko wa kwanza;

APR Rwanda) 0-0 Club Africain (Tunisia)

Al Hilal (Sudan) 4-0 JKU (Zanzibar)

Al-Merrikh (Sudan) 2-1 Vipers (Uganda)

Simba (Tanzania) 4-1 Mbabane Swallows (Eswatini)

Le Messager Ngozi (Burundi) 0-1 Ismaily (Misri)

Mshindi katika mechi za mzunguko wa awali, atafuzu katika hatua ya kwnaza, Timu ambazo zinasuburiwa katika hatua ya kwanza ni pamoja na Wydad Casablanca, TP Mazembe, Al Ahly, AS Vita Club.

 

More in East Africa