Connect with us

African Football

CAF kuamua mgombea wa kumuunga mkono urais wa FIFA

CAF kuamua mgombea wa kumuunga mkono urais wa FIFA

Viongozi wa mchezo wa soka barani Afrika CAF, wanakutana jijini Kigali nchini Rwanda leo Ijumaa katika mkutano muhimu wa kuamua ni mgombea yupi watakayemuunga mkono wakati wa uchaguzi wa urais wa Shirikisho la soka duniani FIFA tarehe 26 mwezi huu.

Wagombea watano wanaowania wadhifa huo. Wanne watakuwa katika mkutano huo ambao, na ni pamoja na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, raia wa Shirikisho la soka barani Asia, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya Gianni Infantino, Mwafrika pekee Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini na Jerome Champagne, aliyekuwa wakati mmoja Naibu Katibu Mkuu wa FIFA.

fifa-elections-2016-1448875807-800

Mgombea mwingine, Mwanamfalme wa Jordan Ali bin al Hussein hatakuwepo katika mkutano huo wa leo lakini aliwahi kukutana na viongozi wa CAF katika siku zilizopita kuomba uugwaji mkono.

Bara la Afrika ambalo lina mashirikisho 54 ya soka ni mdau muhimu wakati wa uchaguzi wa rais wa FIFA, na wadadisi wa soka wanasema atakayepata ungwaji mkono wa bara la Afrika, atakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda urais wa FIFA.

fifa-candidates_getty

Kaimu rais wa FIFA ambaye pia ni kiongozi wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayatou, amenukuliwa akisema kuwa bara la Afrika haliwezi kulazimishiwa mtu wa kumuunga mkono na litafanya uamuzi wake bila shinikizo zozote.

Sepp Blatter ambaye amepigwa marufuku ya kutoshiriki katika maswala ya soka kwa sababu za kimaadili, alijiuzulu kutokana na tuhma za ufisadi katika Shirikisho hilo.

More in African Football