Connect with us

 

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, linatarajiwa kufanya droo ya mzunguko wa tatu, kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Droo hiyo itafanyika katika makao makuu ya Shirikisho hilo mjini Cairo nchini Misri.

Mataifa 20 yatawekwa katika makundi matano, na michuano itachezwa nyumbani na ugenini kati ya mwezi Oktoba mwaka huu na Novemba mwaka 2017.

Mshindi wa kila kundi,atakayepata alama nyingi baada ya mechi zote kukamilika,atafuzu katika fainali hiyo.

Mataifa hayo 20 ni :- Algeria, Burkina Faso, Congo Brazaville, Cote Dvoire, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Cape Verde, Misri, Gabon, Ghana, Guinea, Libya, Morroco, Mali,Nigeria,Afrika Kusini, Senegal,Tunisia, Uganda na Zambia

Cameroon inashikilia rekodi ya kufuzu katika michuano hii mara nyingi zaidi miongoni mwa mataifa ya Afrika, baada ya kufuzu mara 7 mwaka 1982, 1990, 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014.

Nigeria nayo imefuzu mara tano, mwaka 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014.

Mataifa mengine ambayo yamewahi kufuzu ni pamoja na Algeria,Morroco na Tunisia zote mara 4.

Cote Dvoire, Ghana, Afrika Kusini mara 3, Misri mara 2 huku Zaire( DRC), Senegal, Angola na Togo zikifuzu mara 1.

More in