Connect with us

 

Matumaini ya klabu ya soka ya Tanzania Yanga FC kusonga mbele katika michuano ya kuwania taji la Shirikisho barani Afrika, yamefifia baada ya kushindwa kupata ushindi muhimu dhidi ya Medeama SC katika mchuano muhimu uliochezwa Jumamosi jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kuelekea mchuano huu muhimu, ambao Yanga walihitaji kupata ushindi, matumaini yalikuwa makubwa ya angalau kupata ushindi wake wa kwanza lakini mchuano wa leo umemalizika kwa sare ya bao 1 kwa 1.

Yanga FC ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya pili ya mchuano huo bao lilitiwa kimyani Donald Ngoma mchezaji wa kulipwa kutoka Zimbabwe lakini katika dakika ya 17 Medeama ilisawazisha kupitia mshabuliajin wake Bernard Ofori.

Kwa matokeo haya, Yanga inasalia katika nafasi ya mwisho bila ya alama yoyote katika kundi A baada ya kucheza mechi tatu. Ilifungwa na TP Mazembe ya DRC bao 1 kwa 0 sawa na MO Bejaia ya Algeria pia kwa bao 1 kwa 0.

Medeama nayo inasalia katika nafasi ya tatu kwa alama 2.

Marefarii wa mechi hii walikuwa kutoka nchini Misri, wakiongozwa na refa wa katikati Nour El Din.

Kamisaa wa mechi hii amekuwa ni Pasipononga Liwewe kutoka Zambia, huku msimamizi wa marefarii akiwa Mfubusa Bernard pia kutoka Zambia.

Mechi nyingine ya leo katika taji hili la Shirikisho, ni kati ya Etoile du Sahel ya Tunisia dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya saa nne na nusu usiku.

Kesho Jumapili-MO Bejaia ya Algeria itakuwa wenyeji wa TP Mazembe ya DRC kuazia saa 4 na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki.

Klabu bingwa barani Afrika.

Zesco United 3 – ASEC Mimosas 1

Al Ahly ya Misri vs Wydada Casablanca-Saa nne na nusu.

More in