Connect with us

CAF: Michuano ya klabu bingwa na Shirikisho kuanza

CAF: Michuano ya klabu bingwa na Shirikisho kuanza

Michuano ya hatua ya awali, kutafuta ubingwa wa taji la Shirikisho na lile la klabu bingwa barani Afrika inaanza kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika kuanzia siku ya Ijumaa Jumapili.

Klabu ya Vipers nchini Uganda itachuana na Enyimba ya Nigeria jijini Kampala siku ya Ijumaa kuwania taji la klabu bingwa CAF.

Mchuano huo utachezwa kuanzia saa 10 jioni saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Nakivubo.

Vipers wanashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza, huku Enyimba ikiwa na uzoefu katika mashindano haya na iliwahi kunyakua taji hili mwaka 2003 na 2004.

Mshindi wa mchuano huu utakaochezwa nyumbani na ugenini atafuzu katika mzunguko kwa kwanza wa michuano hii na kukutana na Lioli ya Lesotho au Vital’o ya Burundi mwezi Machi.

Klabu nyingine ya Uganda, SC Villa itakuwa ugenini jijini Khartoum kumenyana na Khartoum Watani katika mchuano wa kusaka taji la Shirikisho.

Mshindi baada ya mechi ya mzunguko wa pili mwishoni mwa mwezi huu jijini Kampala, atamenyana na JKU ya Zanzibar au Gaborone ya Bostwana katika mzunguko wa kwanza.

Ratiba ya michuano nyingine:

Klabu Bingwa-Jumamosi Februari 13 2016

Cercle de Joachim (Mauritania ) vs Yanga (Tanzania )

Gor Mahia (Kenya) vs CnaPS Sport (Madagascar)

Mafunzo (Zanzibar) Vs Vita Club (DRC)

Taji la Shirikisho CAF-Jumamosi

Fomboni (Comoros) vs Athletico Olympic (Burundi)

Police (Rwanda) vs Atlabar (Sudan Kusini )

Klabu bingwa-Jumapili

Mbabane Swallows (Swaziland) vs APR (Rwanda)

Taji la Shirikisho-Jumapili

Saint Eloi Lupopo (DRC) vs Bandari ( Kenya)

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in