Connect with us

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limefanya mabadiliko ya siku za kuchezwa michuano ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika.

Michuano ya klabu bingwa sasa itakuwa inachezwa siku za Ijumaa, Jumamosi na siku za Jumanne.

Siku za Jumapili na Jumatano, imetengwa mahsusi kwa ajili ya michuano ya taji la Shirikisho.

Amr Fahmy, Katibu Mkuu wa CAF amesema mabadiliko hayo yanalenga kuwashawishi mashabiki kufika uwanjani kwa wingi lakini kujaribu kuyafanya mashindano hayo kuwa maarufu.

Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa wakati wa michuano ya hatua ya makundi msimu huu.

 

More in