Connect with us

African Football

CAF yamfungia mchezaji wa AS Vita Club

CAF yamfungia mchezaji wa AS Vita Club

 

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limemfungua mchezaji wa AS Vita Club nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Emmanuel Ngudikama, kwa kutumia dawa za kusisimua misuli au kuomgeza nguvu mwilini wakati wa michuano ya Afrika CHAN iliyofanyika nchini Rwanda mapema mwaka huu.

Hata hivyo, CAF haijasema inamfungua mchezaji huyo kwa muda gani.

Ripoti kutoka katika Shirikisho la soka FECOFA, zinasema mchezaji huyo aligunduliwa kutumia dawa hiyo iliyopigwa marufuku na CAF baada ya mchuano wa nusu fainali kati ya DRC na Guinea.

Hii inaamanisha kuwa mchezaji huyo hatoshiriki katika michuano ya klabu yake na timu ya taifa ndani na nje ya nchi hiyo.

Ngudikama  ni miongoni mwa wachezaji 23 walioisaidia DRC kunyakua ubingwa wa CHAN uliofanyika kati ya tarehe 16 mwezi Januari hadi Februari 8 nchini Rwanda.

More in African Football