Connect with us

Shirikisho la soka barani Afrika, limetangaza droo ya hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.

Timu 16 kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika yameratibiwa kuanza kumenyana nyumbani na ugenini kati ya mwezi Mei na Agosti.

Kuna makundi manne, kila kundi na timu nne.

Timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Rayon Sports ya Rwanda, Young Africans ya Tanzania, Gor Mahia ya Kenya na USM Alger ya Algeria, zimepangwa katika kundi la D.

Kundi la C, kuna Enyimba ya Nigeria, Williamsville AC ya Cote Dvoire, CARA Brazzaville ya Congo na Djoliba ya Mali zimepangwa pamoja.

Kundi B, kuna RS Berkane ya Morocco, Al-Masry ya Misri, UD Songo ya Msumbiji na Al-Hilal ya Sudan huku kundi la A, likiwa na ASEC Mimosas ya Cote Dvoire, Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita Club ya DRC na Aduana Stars ya Ghana.

Klabu mbili, ya kwanza na ya pili zitafuzu katika hatua ya robo fainali mwezi Septemba.

Mabingwa watetezi wa taji hili la Shirikisho ni TP Mazembe ya DRC.

More in African Football