Connect with us

Michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika, inarejelewa tena wiki hii katika mataifa mbalimbali.

Viongozi wa kundi B TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watakuwa nyumbani kumenyana na MC Alger ya Algeria.

Mechi hii inakuja baada ya mechi ya mwezi Mei, ambayo iliifunga Difaa El Jadidi ya Morocco mabao 2-0.

Mazembe inaongoza kundi hili kwa alama sita, baada ya kushinda mechi zake zote, huku ikifuatwa na MC Alger ikiwa na alama nne.

KCCA ya Uganda ipo ugenini kumenyana na viongozi wa kundi A, Esperance de Tunis ya Tunisia ambayo ina alama 4, baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare mwingine.

Wawakilishi wa Uganda, wana alama tatu baada ya kuishinda Al Ahly ya Misri mabao 2-0.

Ratiba nyingine:-

Togo Port vs Mamelodi Sundowns

Mbabane Swallows vs Etoile du Sahel

Horoya vs Wydad Casablanca

ES Setif vs Difaa El Jadida

Mbali na michuano hii ya siku ya Jumatano kutakuwa na mechi za kutafuta ubingwa wa taji la Shirikisho.

Majirani, Gor Mahia ya Kenya na Yanga ya Tanzania, watamenyana katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

Gor Mahia watakwenda katika mechi hii baada ya kutokea nchini Tanzania katika mashidano ya CECAFA, walikomaliza katika bafasi ya tatu.

Wawakilishi hao wa Kenya ni wa pili katika kundi D kwa alama 2 baada ya kutoka sare na Rayon Sport bao 1-1 na kutofungana na USM Alger katika mechi zilizopita.

Yanga ambao walisusia michuano ya CECAFA, wamekwenda Nairobi wakiwa na maadalizi mabaya huku Gor Mahia nayo itamkosa aliyekuwa mshambuliaji wake Meddie Kagere ambaye amehamia Simba FC ya Tanzania.

Rayon Sport nao watakuwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali kumenyana na USM Alger.

Ratiba nyingine:-

Aduana Stars vs Vita Club

Enyimba vs WAC

Djoliba vs CARA Brazaville

ASEC Mimosas vs Raja Casablanca

More in African Football