Connect with us

CAF:TP Mazembe kupigia msumari wa mwisho

CAF:TP Mazembe kupigia msumari wa mwisho

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia kesho Jumapili itajitosa katika uwanja wake wa nyumbani mjini Lumbumbashi katika fainali ya pili kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya USM Alger kutoka nchini Algeria.

Mazembe inakwenda katika fainali hii ikiwa na matumaini ya kunyakua taji hilo baada ya kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1 katika fainali ya kwanza mwishoni mwa juma lililopita ugenini.

Mshindi wa kesho mbali na kuwa bingwa wa Afrika, atawakilisha bara la Afrika katika michuano ya dunia baina ya vlabu itakayochezwa nchini Japan mwezi Desemba mwaka huu.

Mazembe ambao wameshinda taji hili mara nne, mwisho ikiwa ni mwaka 2010 ina nafasi kubwa ya kushinda kutokana na rekodi nzuri ya kupata ushindi nyumbani.

Historia inaonesha kuwa kati ya mechi 77 ambazo TP Mazembe imecheza tangu ilipoanza kushiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 1965, imepoteza tu michuano mitatu.

Kocha wa Mazembe Mfaransa Patrice Carteron anaamini kuwa kazi kubwa bado ipo mbele yake na amewaambia wachezaji wake kufanya mashambulizi ili kupata bao la mapema.

USM Alger ambayo imefika katika hatua hii ya fainali kwa mara ya kwanza, itamkosa mchezaji wao wa kutegemewa Youcef Belaili aliyepewa adhabu baada ya kupatikana na kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini na Hocine El Orfi alioneshwa kadi nyekundu.

Mazembe nao watamkosa Rainford Kalaba kutoka Zambia na beki Jean Kasusula anayeuguza jeraha.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in