Connect with us

Cameroon imepanda nafasi 29 katika orodha mpya iliyotolewa na Shirikisho la soka duniani FIFA kuonesha timu bora kwa mwezi wa Februari mwaka 2017.

Hii inakuja baada ya nchi hiyo kunyakua taji la bara Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Gabon, baada ya kuilaza Misri mabao 2-1.

Cameroon kwa sasa ni ya 33 duniani na ya tatu barani Afrika baada ya mafanikio hayo makubwa.

Nafasi ya kwanza kwa sasa barani Afrika imechukuliwa na Misri ambayo ilifika fainali AFCON na imepanda nafasi 12, huku duniani ikiwa ya 23.

Senegal ni ya 31 duniani lakini ni ya pili barani Afrika.

Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inashikilia nafasi ya tano barani Afrika na ya 37 duniani, baada ya kupanda nafasi 12.

Mabingwa wa zamani barani Afrika Cote d’Ivoire, imeshuka nafasi 13 na ni ya tisa barani Afrika na ya 47 duniani.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda ambayo ilicheza katika michuano ya bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, imeshuka nafasi mbili na sasa ni ya 75 barani Afrika laki ya kwanza katika ukanda wa CECAFA.

Kenya inafuata, lakini imesalia katika nafasi ya 87 duniani. Haijapanda wala kushuka.

Rwanda imeshuka nafasi saba, na duniani ni ya 100.

Ethiopia inashikilia nafasi ya 103, baada ya kupanda nafasi 9 huku Burundi ikiwa ya 138 baada ya kupanda tu nafasi moja.

Sudan ni ya 139, huku Tanzania ikishikilia nafasi ya 158 baada ya kushuka nafasi mbili.

Sudan Kusini inashikilia nafasi ya 169 baada ya kushuka nafasi moja.

Somalia, Eritrea na Djibouti zinashikilia nafasi ya mwisho ya 205.

Duniani, Argentina inaongoza, Brazil ya pili, Ujerumani ya Tatu, Chile ya nne na Ubelgiji ya tano. Ufaransa inafunga sita bora duniani.

More in