Connect with us

CECAFA 2015: Ethiopia na Rwanda kufungua dimba la mwaka huu

CECAFA 2015: Ethiopia na Rwanda kufungua dimba la mwaka huu

Michuano ya soka ya timu za taifa kati ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inaanza Jumamosi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Burundi watafungua mashindano hayo kuanzia saa nane mchana saa za Afrika Mashariki dhidi ya Zanzibar huku wenyeji Ethiopia wakimenyana na Rwanda.

Mabingwa watetezi wa taji hili ni Harambee Stars ya Kenya ambao wataanza kutetea taji lao dhidi ya Uganda siku ya Jumapili.

Mchuano mwingine wa Jumapili utakuwa kati ya Somalia na Kilimanjaro Stars ya Tanzania bara.

Malawi imealikwa katika mashindano haya na itaanza michuano hii dhidi ya Sudan siku ya Jumatatu.

Kundi A

Ethiopia, Rwanda, Tanzania na Somalia

Kundi B

Burundi, Kenya, Uganda na Zanzibar

Kundi C

Djibouti, Malawi, Sudan Kusini na Sudan

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in