Connect with us

CECAFA 2015: Kikosi cha Kilimanjaro Stars chafahamika

CECAFA 2015: Kikosi cha Kilimanjaro Stars chafahamika

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.

Kibadeni amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars.

Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.

Wachezaji walioitwa ni Magolikipa:

Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).

Viungo wa Kati:

Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).

Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.

Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in