Connect with us

CECAFA 2015: Kilimanjaro Stars na Uganda Cranes zapata ushindi

CECAFA 2015: Kilimanjaro Stars na Uganda Cranes zapata ushindi

Matumaini ya Zanzibar kufuzu katika hatua ya mwondoano ya michuano ya soka ya CECAFA baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yamedidimia baada ya kupoteza mchuano wake wa pili Jumanne jioni katika uwanja wa Kimataifa wa Awassa nchini Ethiopia.

Uganda Cranes ambayo ilipoteza mchuano wake wa kwanza dhidi ya Kenya, ilipata ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa 0 dhidi ya Zanzibar Heros katika mchuano wa pili wa kundi B.

Kuelekea mchuano huu, kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic alifanya mabadiliko matatu baada ya kufungwa na Kenya mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa kwanza.

Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza, Uganda walikuwa wanaongoza kwa mabao 2 kwa 0 mabao yote yalitiwa kimyani na mshambuliaji matata Farouk Miya ambaye pia alifungwa kwa penalti.

Uganda ilitawala mchezo huo huku kipa wa Zanzibar Mwadini Ali Mwadini akiondolewa uwanjani kwa kupewa kadi nyekudu kwa uchezaji mbaya.

Mabao mengine ya Uganda yalifungwa na Erisa Ssekisambu na Ceaser Okhuti katika dakika 78 ya mchuano huo.

Uganda wanaongoza kundi la B kwa alama tatu kwa sababu ya wingi wa mabao, inafuatwa na Kenya na Burundi ambazo zina alama tatu.

Zanzibar ambayo itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Kenya siku ya Ijumaa haina alama yoyote hadi sasa.

Mchuano mwingine uliochezwa mjini Awasa siku ya Jumanne ni kati ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania bara ambayo iliifunga Amavubi Stars ya Rwanda mabao 2 kwa 1.

Ushindi huu umeipa Tanzania matumai makubwa ya kufika katika hatua ya mwondoano na inaongoza kundi la A kwa alama sita.

Rwanda amabyo ilipata ushindi katika mchuano wake wa kwanza dhidi ya wenyeji Ethiopia, ni wa pili kwa alama tatu huku Ethiopia ikiwa ya tatu na Somalia ya nne.

Siku ya Jumatano, Malawi itamenyana na Djibouti huku Sudan Kusini ikicheza na jirani yake Sudan.

Mchuano mwingine Somalia watamenyana na Ethiopia huku mabingwa watetezi Kenya wakimenyana na Burundi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in