Connect with us

CECAFA 2015: Michuano ya kufuzu hatua ya robo fainali zarejelewa

CECAFA 2015: Michuano ya kufuzu hatua ya robo fainali zarejelewa

Michuano ya soka kuwania taji la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inarejelewa leo Ijumaa nchini Ethiopia baada ya mapumziko siku ya Alhamisi.

Kundi la A, linaloongozwa na Tanzania kwa alama 6, Rwanda alama tatu sawa na Ethiopia.

Rwanda itakuwa na kibarua dhidi ya Rwanda na Somalia ambayo haina alama yeyote baada ya kucheza michuano miwili.

Utakuwa ni mchuano muhimu kwa Amavubi Stars ya Rwanda ambayo inataka kuungana na Tanzania kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Tanzania itacheza na Ethiopia siku ya Jumamosi kutamatisha mechi za kundi hilo.

Zanzibar ambayo tayari wameshaondolewa katika kundi la B, watachuana na mabingwa watetezi Harambee Stars ya Kenya ambayo inaongoza kundi hilo kwa alama 4 sawa na Burundi ambayo itacheza na Uganda siku ya Jumamosi katika uwanja wa Awassa.

Michuano ya kundi C inamalizika siku ya Ijumaa, Sudan Kusini ambayo ni ya pili kwa alama 4, na itachuana na Malawi ambayo inaongoza kundi hilo kwa alama 6 na tayari imeshafuzu katika hatua ya mwondoano.

Djibouti ambayo imeshaondolewa katika michuaono hii itachuana na Sudan ambayo ina alama 1 baada ya mchuano huo.

Michuano ya robo fainali itaanza kuchezwa siku ya Jumatatu juma lijalo.

Advertisement

Must See

More in