Connect with us

Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, bado halijapata mwenyeji wa michuano ya mwaka huu kuwania taji la Kagame, ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika kati ya tarehe 18 mwezi Juni na kumalizika mwezi Julai tarehe 2 nchini Tanzania.

Shirikisho la soka nchini Tanzania lilikataa kuwa wenyeji wa makala haya ya 41, kwa kile walichokisema kuwa ilikuwa na michuano ya Kimataifa huku nchi za Sudan na Rwanda ambazo zilikuwa zimeombwa kuchuku nafasi zikisalia kimya hadi sasa.

Msemaji wa CECAFA Rogers Mulindwa, amebaini kuwa Sudan na Rwanda hawatakuwa wenyeji wa michuano hii ambayo imekuwa ikidhaminiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame tangu mwaka 2002.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA) Vincent Nzamwita amesema kuwa hajapata mawasiliano yoyote kutoka kwa CECAFA kuhusu michuano hii.

Kuwa mweyeji wa michezo, hii kunahitaji maandalizi ya muda mrefu na uamuzi wa wadau wote wa soka,” alisema Nzamwita.

Mara ya mwisho Rwanda kuandaa michuano hii ilikuwa ni mwaka 2014, baada ya kufanya hivyo mara nne mwaka 2000, 2004 na 2007.

Tanzania imewahi kuwa wenyeji mara 12 huku Sudan ikiwa wenyeji mara 5.

More in