Connect with us

 

Kenya na Burundi zinamenyana katika mchuano wa pili kuwania taji la CECAFA kwa upande wa wanawake, michuano inayoendelea nchini Uganda.

Mataifa haya mawili yanacheza mechi yao ya pili baada ya kushinda mechi za ufunguzi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mshindi kati ya Kenya na Burundi, atafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Mechi ya kwanza Kenya iliishinda wenyeji Uganda mabao 4-0, huku Burundi wakipata ushindi mkubwa wa mabao 10-1 dhidi ya Zanzibar.

Mchuano mwingine unaochezwa siku ya Jumanne, katika taasisi ya FUFA Njeru mjini Jinja ni kati ya wenyeji Uganda na Zanzibar.

Siku ya Jumatatu, Kilimanjaro Queens ya Tanzania bara iliishinda She-Amavubi ya Rwanda katika mchuano wa kundi B kwa mabao 3-2 .

Tanzania walianza vema kwa kupata mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza, mabao waliyofungwa na Asha Rashid na Stumai Abdalla.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye Rwanda ilirejea na kusawazisha mabao yote kupitia na Anne Marie na Anton Anastazia lakini baadaye Tanzania ikajipatia bao la ushindi katika dakika za lala salama.

Ratiba

Jumatano Septemba 14 2016

  • Rwanda vs Ethiopia

Alhamisi Septemba 15 2016

  • Kenya vs Zanzibar

  • Uganda vs Burundi

Mechi za nusu fainali zitachezwa siku ya Jumamosi, Septemba tarehe 17 huku fainali ikipigwa siku ya Jumatatu tarehe 19.

Michuano hii inachezwa kwa mara ya pili kwa muda mrefu baada ya Zanzibar kuandaa michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986.

 

More in African Football