Connect with us

African Football

CHAN 2016: Mali kumenyana na DRC fainali

CHAN 2016: Mali kumenyana na DRC fainali

hi-res-3cbeaa104b284b5c071a774929966c83_crop_north

Mali itachuana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika fainali ya mchezo wa soka kuwania ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN.

Mali ilifuzu siku ya Alhamisi baada ya kuifunga Ivory Coast katika mchuano wa nusu fainali jijini Kigali nchini Rwanda.

Yves Bissoouma ndiye mchezaji aliyeipa Mali bao la ushindi katika dakika ya 88 ya mchuano huo mgumu.

Baada ya mchuano huo, kocha wa Mali Djibril Drame amekiri kuwa timu ya DRC ni timu nzuri na anatambua mabingwa wa kwanza wa CHAN mwaka 2009 lakini, wachezaji wake hawaiogopi.

Aidha, Mali inajivunia idadi kubwa ya vijana chipukizi, kama Sekou Koita ,Abdoul Karim Dante, Mousa Sisoko na Mamadou Doumbia.

aiglonnet-joueur-coupe-mondiale-cadets-junior

Nayo Leopard, kwa upande wake inajivunia wachezaji wengine wenye uzoefu wanaochezea klabu ya TP Mazembe, Vita Club na DC Motema Pembe wakiongozwa na nahodha Joël Kimwaki Mpela .

Maelfu ya mashabiki wa DRC pia wanatarajiwa kushuhudia mchuano huo kuishabikia Leopard.

DRC plaYERS

Fainali itachezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Amahoro lakini itatanguliwa na mchuano kati ya Tembo wa Ivory Coast na Syli National ya Guinea kumtafuta mshindi wa tatu.

 

More in African Football