Connect with us

Chipolopolo (Zambia)

CHAN 2016: Oliseh aomba radhi baada ya Nigeria kuondolewa

CHAN 2016: Oliseh aomba radhi baada ya Nigeria kuondolewa

Sunday Oliseh_4

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Sunday Oliseh amewaomba msamaha mashabiki wa soka katika nchi yake baada ya Super Eagles kuondolewa katika hatua ya makundi ya michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza nyumbani CHAN.

Nigeria iliondolewa siku ya Jumanne baada ya kufungwa na Guinea inayoshiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza bao 1 kwa 0.

Bao pekee la Guinea lilitiwa kimyani na Ibrahim Sankhon katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Tunawaomba msamaha raia wa Nigeria kwa kupoteza mchuano huu, vijana walijitahidi lakini hawakufanikiwa,” alisema Oliseh.

BDE40BDADF38194C0F3198D8968E9E5A

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini humo NFF Amaju Pinnick, amesisitiza kuwa mashindano ya CHAN yalinuiwa kuwapa nafasi wachezaji wa nyumbani na kuwasaidia kujiandaa kushiriki katika michuano ijayo hasa ile ya kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017.

Aidha, amewapongeza wachezaji wote wa Super Eagles na kuwataja wachache kama Usman Mohammed, Chima Akas, Ikechukwu Ezenwa, Austin Oboroakpo na Ifeanyi Mathew walionekana kucheza vizuri katika michuano hii hiyo.

Nigeria imeondoka katika michuano hii huku Chisom Chikatara, akiweka historia kwa kuifungia timu yake mabao 4 na kuwa mfungaji bora katika hatua ya makundi.

default

Mwaka 2014, Nigeria iliposhiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano haya yalipoandaliwa nchini Afrika Kusini, walimaliza katika nafasi ya tatu.

Tunisia pia imefuzu kutoka kundi C baada ya kuishinda Niger mabao 5 kwa 0.

Guinea sasa inasubiri mshindi wa kundi D, kupambana naye katika hatua ya robo fainali huku Tunisia ikisubiri mshindi wa pili wa kundi hilo.

Nayo michuano ya kutamatisha kundi la D inachezwa siku ya Jumatano jioni.

Image

Uganda inamenyana na Zimbabwe ambayo imeshaondolewa katika michuano hii katika uwanja wa Umugunda mjini Gisenyi, huku Zambia wakipambana na Mali katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali.

Michuano yote inachezwa kwa pamoja kuanzia saa 10 Kamili saa za Afrika ya Kati.

Zambia inaongoza kundi hilo kwa alama 6, Mali ni ya pili kwa alama 4, Uganda alama 1 na Zimbabwe haina alama yoyote.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in Chipolopolo (Zambia)