Connect with us

CHAN 2016: Rwanda na Cameroon kucheza mechi ya kirafiki

CHAN 2016: Rwanda na Cameroon kucheza mechi ya kirafiki

Timu ya taifa ya soka ya Cameroon imewasili jijini Kigali nchini Rwanda kushiriki katika michuano wa Kimataifa wa kirafiki siku ya Jumatano wiki hii.

Mchuano huo utachezwa katika Wilaya ya Rubavu na mchuano huo ni maandalizi ya fainali za CHAN, michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani.

Mashindano haya yataanza tarehe 16 mwezi huu nchini Rwanda.

Amavubi Stars imekuwa ikipiga kambi katika Wilaya ya Rubavu tangu mwisho wa mwaka uliopita kwa maandalizi ya mashindano haya na kujiandaa dhidi ya Cameroon.

Kikosi cha Cameroon: Hugo Patrick Nyame, Pierre Sylvain Abodo, Derrick Anye Fru, Mohammed Djetei, Aaron Mbimbe, Yves Robert Chouake, Joseph Jonathan Ngwem, Alexandre Kombi Mandjang, Carlain Manga Mba, Nicolas Joel Owona Mbassegue, Stephan Kingue Mpondo, Paul Serge Atangana Mvondo,Guy Christian Zock, Samuel Oum Douet, Moumi Ngamaleu, Ghislain Moguu, Ambane Moumourou Idriss, Mark Nkongho Ojong, Yazid Atouba Emane, Lionel Ngondji, Moussa Souleymanou, Samuel Nlend, Harouna Mahamat, Ronald Ngah, Frank Boya and Junior Mfede.

Rwanda iko katika kundi moja na Gabon, Moroco na Cote Dvoire huku Cameroon ikiwa katika kundi la B na DRC, Angola na Ethiopia.

Mataifa 16 yatashiriki katika michuano hii ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili tangu mwaka 2009.

Michuano hiyo itachezwa katika viwanja vinne, uwanja wa Amahoro jijini Kigali ulio na uwezo wa kuwakaribisha mashabiki elfu 30.

Uwanja wa Nyamirambo ambao pia upo jijini Kigali, uwanja wa Butare na ule wa Gisenyi.

Mataifa yaliyofuzu ni pamoja na wenyeji Rwanda, Uganda, DRC, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Angola, Gabon, Cameroon, Nigeria, Niger, Ivory Coast, Mali, Guinea, Tunisia na Morocco.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in