Connect with us

CHAN 2016: Rwanda yaondoa ada ya Visa kwa mashabiki wa soka

CHAN 2016: Rwanda yaondoa ada ya Visa kwa mashabiki wa soka

Michuano ya soka ya CHAN kuwania ubingwa wa Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani, intarajiwa kuanza Jumamosi ijayo tarehe 16 mwezi huu nchini Rwanda.

Mataifa 15 pamoja na Rwanda yatashiriki katika michuani hii inayitarajiwa kuwakusanya maelfu ya wapenzi wa soka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

1451771741amavubi-training

Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa hakutakuwa na malipo ya Visa kwa mashabiki wa mataifa yatakayoshiriki katika michuano hii watakaoamua kwenda nchini humo kuzishabikia timu zao.

Hii inamaana kuwa idadi kubwa ya mashabiki wanatarajiwa kushiriki katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda.

Katibu katika Wizara ya Michezo Edward Kalisa, amesema,”Tumeondoa ada ya kupata Visa kwa wachezaji, mashabiki na wajumbe wa CAF kutoka mataifa yote yanayoshiriki katika michuano hii,”.

Tunaamini kuwa hatua hii ya serikali itasababisha kuwepo kwa mashabiki wengi na hata kuongeza utalii nchini Rwanda na tayari tuna hoteli za kutosha kuwapokea wageni watakaokuja,” aliongeza.

Uwanja wa soka Rubavu

Wiki hii kumekuwa na michuano ya kirafiki kwa maandalizi ya michuano hii, weyeji Rwanda wakicheza wiki hii na Cameroon walitoka sare ya bao 1 kwa 1.

Angola nao walipambana na Nigeria nchini Afrika Kusini na pia kutoka sare ya bao 1 kwa 1.

Siku ya Jumapili, kutakuwa na michuano kadhaa ya kirafiki kuendelea kujiandaa kwa michuano hii, Angola watacheza na Guinea, Uganda watamenyana na Gabon, huku Rwanda wakijipima nguvu na jirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mataifa yatakayoshiriki ni pamoja na:Wenyeji Rwanda, Uganda, Ethiopia, Zimbabwe, Zambia, Angola, Gabon, Cameroon, DR Congo, Niger, Nigeria, Ivory Coast, Guinea, Mali, Tunisia na Morocco.

Mabingwa wa taji hili:-

DR Congo-2009 Michuano iliandaliwa nchini Cote D’voire

Tunisia-2011 Michuano iliandaliwa nchini Sudan

Libya-2014 Michuano iliandaliwa nchini Afrika Kusini

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in