Connect with us

African Football

CHAN 2016: Uchambuzi wa kundi B

CHAN 2016: Uchambuzi wa kundi B

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayowajumuisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani, Itaanza kuwani ubingwa wa michuano ya Afrika CHAN, dhidi ya Ethiopia siku ya Jumapili katika uwanja wa Huye mjini Butare.

Leopard imeshiriki katika makala yote ya CHAN tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 nchini Cote D’voire, mwaka ambao waliibuka mabingwa wa kwanza wa taji hili.

Kocha Florent Ibenge amesema anafahamu kuwa kundi la B ni gumu lakini, vijana wake wamejiandaa vya kutoka na wana uwezo wa kunyakua ubingwa wa mwaka huu.

Léopards-de-la-RDC

Mwishoni mwa juma lililopita, Leopard ilifungwa na Amavubi Stars ya Rwanda bao 1 kwa 0 katika mchuano wa kirafiki kwa maandalizi ya michuano huu.

Mashabiki wa DRC wanatarajiwa kufurika nchini Rwanda kushuhudia michuano hii hasa baada ya serikali ya Rwanda kuondoa malipo ya Visa kwa mashabiki wa timu zinazoshiriki katika michuano hii ya CHAN.

Kikosi cha DRC:

Kipa: Matampi Vumi

Mabeki : Bahumeto, Bompunga Botuli, Kimwaki Mpela Joël, Lomalisa Mutambala

Viungo wa Kati : Munganga Omba, Doxa Gikanji , Ricky Tulengi , Lusadisu Basisila, Cédric Ngulubi

Washambuliaji : Luvumbu Nzinga, Bolingi Mpangi, Mechak Elia

DR Congo fan during the 2013 Orange Africa Cup of Nations football match, Ghana Vs DR Congo at the Nelson Mandela Bay Stadium in Port Elizabeth, South Africa on January 20, 2013. Photo by Sports Inc/PA Photos/ABACAPRESS.COM

Kundi hili pia lina mataifa mengine ya Angola na Cameroon.

Angola inashiriki kwa mara ya pili katika mashindano haya na mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2011, walikomaliza katika nafasi ya pili baada ya kufungwa katika mchuano wa fainali na Tunisia mabao 3 kwa 0 wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Sudan.

Cameroon nayo inashiriki katika michuano hii kwa mara ya pili na mwisho ilikuwa ni mwaka 2011 walikoondolewa katika hatua ya robo fainali.

Mwishoni mwa juma lililopita, katika mchuano wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa mashindano haya Rwanda, timu zote mbili zilitoka sare ya bao 1 kwa 1.

Ethiopia inashiriki pia kwa mara ya pili, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 wakati michuano hii ilipofanyika nchini Afrika Kusini na ikaondolewa katika hatua ya makundi.

Mchuano wa kirafiki kati ya vijana wa Walia Ibex na Niger kwa maandalizi ya michuano hii, ilitoka sare ya bao 1 kwa 1.

More in African Football