Connect with us

African Football

CHAN 2016: Uganda na Burundi waanza vema nyumbani

CHAN 2016: Uganda na Burundi waanza vema nyumbani

Michuano ya soka kufuzu kucheza katika fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN mwaka ujao, inachezwa mwishoni mwa juma hili katika mataifa mbalimbali.

Timu ya Taifa ya Uganda ilianza vema mchuano wake wa kwanza siku ya Jumamosi ikiwa nyumbani jijini Kampala baada ya kuishinda Sudan mabao 2 kwa 0.

Mabao ya Cranes yalitiwa kimyani na nahodha Farouk Miya, katika dakika 36 kabla ya muda wa mapumziko kipindi cha kwannza huku Frank Kalanda akifungua ukurasa huo katika dakika 19 ya mchuano huo.

Burundi nao ilianza vema kampeni yao ya kufuzu baada ya kuifunga Ethiopia pia kwa mabao 2 kwa 0 katika mchuano uliochezwa jijini Bujumbura.

Michuano ya marudiano itachezwa mwishoni mwa juma lijalo na mshindi atafuzu katika fainali za michuano hiyo itakayoandaliwa nchini Rwanda mwaka ujao.

Matokeo Kamili ya siku ya Jumamosi

Uganda 2 Sudan 0

Burundi 2 Ethiopia 0

Zambia 3 Mozambique 0

Afrika Kusini 0 Angola 2

Niger 2 Togo 0

Michuano ya Jumapili

Cameroon Vs Congo

Chad Vs Gabon

Mali Vs Mauritania

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu baada ya Jamhuri ya timu ya Afrika ya Kati kujiondoa kwa kile ilichosema kuwa haina fedha ya kuendelea na mashindano haya.

 

More in African Football