Connect with us

CHAN 2016:Uchambuzi Ethiopia dhidi ya Kenya

CHAN 2016:Uchambuzi Ethiopia dhidi ya Kenya

Na Victor Abuso,
Timu ya taifa ya soka ya Ethiopia Walia Ibex , inajiandaa kumenyana na Harambee Stars ya Kenya Jumapili hii katika mchuano wa kufuzu katika michuano ya Afrika ya CHAN baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani mwaka ujao.

Ethiopia na Kenya wamekutana mara 34 katika michuano ya Kimataifa tangu mwaka 1962, na Ethiopia ilifuzu katika michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2014 wakati ilipoandaliwa nchini Afrika Kusini.

Mchuano wa Jumapili ni muhimu kwa timu zote mbili ambazo zinalenga kufuzu katika michuano ya mwaka 2016 utakaofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.

Hadi sasa Shirikisho la soka nchini Ethiopia, EFF halijatangaza ni uwanja upi utakaotumiwa katika mchuano huo lakini kuna uwezekano ukachezwa katika uwanja wa Bahirday ambao walioutumia dhidi ya Lesotho katika mchuano wa kufuzu wa mataifa bingwa barani Afrika mwishoni mwa juma lililopita.

Kocha wa Ethipia Yohannes Sahle anawategemea wachezaji kama Behailu Assefa aka Tusa kiungo wa kati anayechezea klabu ya St.Georges ambaye amekuwa muhimu sana katika kikosi cha taifa tangu michuano ya CHAN mwaka 2014.

Wachezaji wengine wa kutegemewa ni pamoja na beki Salhadin Bargecho huku safu ya mashambulizi ikiongozwa na Biniyam Assefa pamoja na Baye Gezahegn.

Kwa upande wa Harambee Stars ambayo haijawahi kufuzu katika michuano hii, kocha Bobby Williamson anatarajiwa kuwa na wachezaji wanne waliokuwa katika kikosi kilichomenyana na Congo Brazaville katika michuano ya kufuzu kwa michezo ya Afrika mwaka 2017.

Wachezaji hao ni pamoja na kipa Bonface Oluoch ambaye pia anaichezea Gor Mahia, Collins Okoth Gattuso na Michael Olunga.

Washambualiaji wa kutegemewa ni pamoja na Jesse Were na Michael Olunga ambao wanaongoza katika safu ya ufungaji mabao katika ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL.

Kocha Williamson anatarajiwa kutumia mfumo wa 4-4-2 ambao anaamini unaweza kumletea ushindi ugenini Jumapili hii.

Baada ya mchuano wa Jumapili hii, Kenya na Ethiopia zitarudiana tena jijini Nairobi mapema mwezi ujao kuamua hatima ya timu itakayosonga mbele.

 

 

 

 

Kikosi cha Ethiopia

Mfumo: 4-4-2

Kipa: Tarik Getnet(Dedebit)

Mabeki: Zekarias Tuji(St.George), Aschalew Tameme(Dedebit), Salhadin Bargecho(St.George), Siyoum Tesfaye(Dedebit)

Kiungo wa Kati: Behailu Assefa(St.George), Gatoch Panom(Ethiopia Bunna), Firew Solomon(Defence) and Aschalew Girma( Ethiopia Bunna)

Washambuliaji: Baye Gezahegn (Wolaitta Dicha) and Biniam Assefa (Ethiopia Bunna)

 

Kenya Harambee Stars

Mfumo: 4-4-2

Kipa: Bonface Oluoch(Gor Mahia)

Mabeki: Edwin Wafula(AFC Leopards),Lloyd Wahome(Tusker),Aboud Omar(Unattached) Jackson Saleh(AFC Leopards)

Kiungo wa Kati :Collins Okoth Gattuso(Gor Mahia),Humphrey Mieno(Tusker)Victor Ali Abondo(Gor Mahia) and Kevin Kimani (Tusker)

Washambuliaji: Jesse Were(Tusker) and Michael Olunga(Gor Mahia)

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in