Connect with us

CHAN 2016:Uganda yajiandaa kukabiliana na Tanzania

CHAN 2016:Uganda yajiandaa kukabiliana na Tanzania

Na:Victor Abuso,

Timu ya taifa ya soka ya Uganda yenye wachezaji wanaocheza soka nyumbani imeanza maandalizi ya michuano ya mzunguko wa kwanza kufuzu kwa michuano ya Afrika CHAN itakayofanyika mwakani nchini Rwanda.

Uganda inajiandaa kuchuana na Tanzania siku ya Jumamosi mchuano utakaochezwa katika visiwa vya Zanzibar.

Kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic anasema baada ya mchuano wa mwishoni mwa juma lililopita wa kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017, kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuikabili Tanzania.

Siku ya Jumanne,kikosi cha Micho kinaendelea na maandalizi yake katika Taasisi ya mafunzo ya kiufundi ya Njeru ili kupata uzoefu katika uwanja wa bandia.

Kikosi kamili:


Makipa:Alitho James, Ochan Benjamin, Bwete Brian

Mabeki: Okoth Denis, Ntambi Julius ,Ochwo Brian, Musisi Farouk, Waswa Hassan, Bakaki Shafiq, Kiyemba Ibrahim, Okello Silvester

Viungo wa Kati: Bukenya Deus, Tekkwo Derrick, Mugerwa Yasser, Kizito Keziron, Mutyaba Muzamil, Eturude Abel, Kyeyune Saidi, Miya Farouk, Kiiza Martin

Washambuliaji: Sekisambu Erisa, Semazi John, Kalanda Frank, Ssentongo Robert, Fahad Muhamed Hassan

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, limempa kocha wa Stars Mart Nooij raia wa Uholanzi nafasi ya mwisho ya kuhakikisha kuwa kikosi chake kinafuzu katika michuano hii, la sivyo ajiuzulu.

Uamuzi huu ulitolewa na uongozi wa soka nchini humo baada kumalizika kwa michuano ya Kusini mwa mataifa ya Afrika COSAFA mwezi mmoja uliopita walikofungwa michuano yao yote.

Tanzania iliwahi kucheza katika michuano hii ya CHAN mwaka 2009 wakati makala ya kwanza ya michuano hii ilipofanyika nchini Cote Dvoire.

Kikosi cha Tanzania:

Salum Swedi, Kelvin Yondani, Amir Maftah, Juma Jabu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Shadrack Nsajigwa na Erasto Nyoni, huku viungo ni Nizar Khalfan, Shaaban Nditi, Mwinyi Kazimoto, Godfrey Bonny, Athuman Idd ‘Chuji’, Nurdin Bakary na Henry Joseph. Safu ya ushambuliaji ilikuwa chini ya Abdi Kassim ‘Babi’, Haruna Moshi ‘Boban’, Kigi Makassy, Mrisho Ngassa, Jerson Tegete, Mussa Hassan Mgosi.

Mbali na Uganda mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Kati yanayojiandaa kufuzu michuano hiyo ya CHAN ni pamoja na Djibouti itakayomenyana na Burundi na Ethiopia na Kenya.

Washindi katika hatua hii watafuzu katika mzunguko wa pili kujiunga na Sudan ambayo imekwishafuzu kutoka ukanda wa CECAFA.

Rwanda wamefuzu kwa sababu ni wenyeji wa michuano hii.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in