Connect with us

CHAN 2016:Wajumbe wa CAF kuzuru Rwanda

CHAN 2016:Wajumbe wa CAF kuzuru Rwanda

Na: Victor Abuso,

Wajumbe wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, wanatarajiwa kuwasili nchini Rwanda kuthathmini tena maandalizi ya nchi hiyo kuelekea fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka katika vlabu vya nyumbani CHAN .

Rwanda inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya Afrika kati ya Januari tarehe 16 hadi Februari tarehe 7mwaka ujao wa 2016.

Wajumbe hao wa CAF watakuwa nchini Rwanda kati ya tarehe 23 hadi 28 mwezi huu na kuchunguza hoteli zitakazotumiwa na wageni wakati wa michuano hiyo pamoja na viwanja vitakavyotumiwa.

Almamy Kabele Camara naibu rais wa CAF, anatarajiwa kuongoza wajumbe wenzake kuzuru viwanja vya Amahoro, Huye na Umuganda katika wilaya ya Rubavu vinavyotarajiwa kufanyika kuandaa michuano hiyo.

Mataifa 15 yatakayofuzu katika fainali hiyo yatabainika baada ya kumalizika kwa michuno ya kufuzu mwezi Oktoba.

Mara ya kwanza kufanyika kwa michuano hii ilikuwa ni mwaka 2009 nchini Cote Dvoire ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa bingwa.

Makala ya pili yalifanyika mwaka 2011 nchini Sudan huku yale ya tatu yakifanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2014.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in