Connect with us

Morocco inarejea dimbani Jumatano usiku dhidi ya Guinea katika mchuano wake wa pili, kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani.

Mchuano huu utachezwa katika uwanja wa Mohamed wa tano mjini Casablanca.

Wenyeji wanakwenda katika mchuano huu wa pili wa kundi A, baada ya kuanza vema kwa kuishinda Mauritania mabao 4-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Guinea nayo ilianza vibaya baada ya kufungwa na Sudan mabao 2-1 na inahitaji ushindi wa leo ili kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Mchuano mwingine wa kundi hili ni Sudan dhidi ya Mauritania ambayo itakuwa inajaribu kutafuta ushindi wake wa kwanza katika michuano hii.

Ratiba inayosalia kundi A, Januari 21 2018:-

Sudan v Morocco

Mauritania v Guinea

Jumanne usiku, Cameroon ilianza vibaya baada ya kufungwa na Congo Brazaville bao 1-0, mechi iliyochezwa katika uwanja wa Adrar mjini Agadir.

Ushindi huo wa Congo ulikuja kupitia Junior Makiesse kupitia mkwaju wa penalti katika dakika 73 ya mchuano huo.

Congo inaongoza kundi la D kwa alama 3 huku Angola na Burkina Faso ikiwa na alama moja baada ya kutofungana katika mchuano huo.

Ratiba Januari 18 2018:-Kundi B

Ivory Coast v Zambia

Uganda v Namibia

Ratiba Januari 19 2018:-Kundi C

Libya v Nigeria

Rwanda v Equitorial Guinea

More in