Connect with us

CHAN:Williamson ataja kikosi tayari kuikabili Ethiopia

CHAN:Williamson ataja kikosi tayari kuikabili Ethiopia

Na Victor Abuso,
Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Bobby Williamson amekitaja kikosi cha wachezaji wanaosakata soka nyumbani kuanza maandalizi ya mchuano wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Ethiopia kufuzu katika michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Rwanda mwakani.

Harambee Stars itakuwa ugenini jijini Addis Ababa kumenyana katika mchuano huo wa kwanza kabla ya kurudiana jijini Nairobi mapema mwezi ujao.

Kikosi cha Williamson kimewajumuisha wachezaji walioachwa wakati wa mchuano wa kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika dhidi ya Congo Brazaville mwishoni mwa juma lililopita.

Wachezaji walioachwa na wameitwa ni pamoja na kiungo wa kati wa Gor Mahia Ali Hassan Abondo na mshambuliaji wa AFC Leopards Jacob Keli.

Kikosi kamili:
Makipa: Boniface Oluoch (Gor Mahia), Ian Otieno (Posta Rangers), Boniface Baraza (Posta Rangers),

Mabeki :  Edwin Wafula (AFC Leopards), Brian Birgen (Ulinzi Stars), Sammy Meja (Thika United), David Gateri  (Bandari), Aboud Omar (Unattached), Jackson Saleh (AFC Leopards), Musa Mohamed (Gor Mahia)

Kiungo wa Kati:  Ali Abondo (Gor Mahia), Kevin Kimani (Tusker), Collins Okoth (Gor Mahia), Humphrey Mieno (Tusker),  Anthony  Ndolo (Sofapaka),  Bernard Mang’oli , Timonah Wanyonyi  (AFC Leopards) Eric Johanna  (Mathare United)

Washambuliaji :  Michael Olunga (Gor Mahia), Jesse Were (Tusker), Peter Nzuki (Nakumatt) , Jacob Keli, Noah Wafula, (AFC Leopards)

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in