Connect with us

Constant Omari Selemani amechaguliwa tena kuwa rais wa Shirikisho la soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, FECOFA.

Uchaguzi huu umefanyika wakati wa mkutano mkuu wa chama cha soka nchini humo uliofanyika siku ya Jumamosi.

Omari ambaye pia ni makamu wa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, hakuwa na mshindani yeyote katika Uchaguzi huo.

Wajumbe wote 28, waliopiga kura, walimpa kura zote na sasa ataongoza tena soka nchini humo kwa muda wa miaka minne ijayo.

Rais huyo wa FECOFA, ameahidi kuendeleza maendeleo ya soka nchini DRC na kuwashukuru wajumbe kwa kuendelea kumwamini.

More in African Football