Connect with us

Zambia na Cameroon zitamenyana katika hatua ya nusu fainali, kuwania taji la COSAFA kwa upande wa wanawake, katika fainali ya mwaka 2018 inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Wolfson mjini KwaZekele nchini Afrika Kusini.

Wenyeji Afrika Kusini nao watapambana na Uganda.

Uganda ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga Zimbabwe mabao 2-1 katika mechi ya mwisho ya kundi C.

Mechi nne ilizocheza, ilishinda mechi mbili, ikatoka sare mara mora moja na kupoteza mechi.

Afrika Kusini nayo iliongoza kundi la A, kwa alama tisa baada ya kushinda mechi tatu dhidi ya Bostwana, Malawi na Madagascar.

Fainali hiyo itachezwa mwishoni mwa wiki hii.

More in