Connect with us

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast Didier Drogba, amesema anastaafu kucheza soka, baada ya zaidi ya miaka 20 katika viwanja vya mchezo huu.

Drogba mwenye umri wa miaka 40, anastaafia katika klabu ya  Phoenix Rising nchini Marekani.

Alianza kucheza ya kulipwa mwaka 1998 katika klabu ya Le Mans nchini Ufaransa, kabla ya kuhamia  klabu ya Guingamp na baadaye Marseille.

Hata hivyo, nyota yake ilingaa sana alipokuwa katika  klabu ya Chelsea nchini Uingereza, alikofunga mabao 164 katika mechi 341 alizocheza.

Aliichezea timu yake ya taifa kati ya mwaka 2002-2014 na kuichezea mechi 104 na kufunga magoli 65, rekodi ambayo bado anaishikilia.

More in