Connect with us
Dirisha la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili msimu wa 2018/2019 limefunguliwa rasmi.
Dirisha hilo limefunguliwa Juni 15,2018 na litafungwa July 26,2018 kwa kutumia mfumo mpya wa usajili(TFF FIFA CONNECT).
Baada ya Dirisha kufungwa kutakuwa na wiki moja ya pingamizi kuanzia July 27,2018 ikifuatiwa na Kamati ya Katiba,Sheria na Hadhi za Wachezaji kukaa kupitisha usajili.
Aidha kuanzia kutakuwa na mafunzo ya mfumo mpya wa usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili yatakayoanza Jumatatu Juni 25,2018 mpaka Jumatano Juni 27,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Hakutakuwa na nafasi nyingine ya mafunzo baada ya mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku moja kwa kila Ligi yakianza na klabu za Ligi Kuu Jumatatu Juni 25,2018.
Kutokana na Changamoto za utumiaji mfumo huo TFF itaendesha mafunzo hayo kwa siku hizo tajwa ili kuhakikisha ufanisi mkubwa katika usajili wa msimu huo mpya.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa