Connect with us

Klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara imethibitisha kuingia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Platnum FC ya Zimbabwe na Yanga, Donald Ngoma.

Kwa muda mrefu msimu uliopita, Ngoma alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha na hivyo kushindwa kuitumikia timu yake ya Yanga katika michuano ya Ligi Kuu na ile ya kimataifa. Licha ya kuwa alikuwa amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, klabu hioyo ilitangaza kuvunja mkataba wake.

Ngoma anajiunga na Azam akiwa ameitumikia Yanga kwa miaka mitatu na kuiwezesha kushinda taji la Ligi Kuu mara mbili mfululizo 2015/2016 na 2016/2017.

Kupitia ukarasa wake katika mtandao wa Instagram, Azam imesema imeingia makubaliano na mchezaji huyo na muda wowote kutoka sasa ityampeleka katika Hospitali ya Vincent Palloti ya Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afyaili kuona namna gani majeraha yaliyokuwa yakimkabili yamepona.

Azam imesema huenda mchezaji huyo akaonekana katika michuano ya Kombe la Kagame inayotazamiwa kuchezwa mwezi ujao nchini Tanzania ikishirikisha klabu kutoka ukanda wa Afrika mashariki na kati.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in