Connect with us

DRC: DC Motema Pembe kuchuana na Vita Club Jumapili

DRC: DC Motema Pembe kuchuana na Vita Club Jumapili

Klabu ya DC Motema Pembe itachuana Jumapili na Vita Club katika mchuano muhimu wa marudiano kuwania taji la taifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa Kimataifa wa Tata Raphael jijini Kinshasa kwa mujibu wa Wizara ya michezo nchini humo.

Mchuano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa timu hizo mbili ambazo zina wafuasi wengi hasa jijini Kinshasa.

Kutokana na upinzani mkali wa mashabiki wa timu hizi mbili na mauaji ya mashabiki wakati wa mchuan kama huu kati ya TP Mazembe na Vita Club mwaka 2014, mashabiki wa timu zote mbili watatumia malango tofauti kuingia uwanjani.

Mchuano wa mzunguko wa kwanza miezi kadhaa iliyopita, DC Motema Pembe iliifunga Vita Club bao 1 kwa 0.

Mwamuzi wa kati wa mchuano huo atakuwa ni Makombo Neushiye, akisaidiwa na Fila Kimfumu, Washe Mukanga na Angova Bongo.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in