Connect with us

DRC na Zimbabwe zakata tiketi AFCON 2019

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu katika fainali ya mchezo wa soka kwa mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liberia katika uwanja wa Tata Raphael jijini Kinshasa.

Mechi hiyo ilikuwa ni muhimu sana kwa Leopard kupata ushindi ili na bao la Cedric Bakamu lilitosha kuwafikisha vijana wa Florient Ibenge katika fainali yao ya 19.

Pamoja na DRC, Zimbabwe nayo imefuzu baada ya kuilaza Congo Brazaville mabao 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Harare.

Brave Warriors walipata ushind huo kupitia, wachezaji wake Khama Billiat katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza, huku Knowledge Musona katika dakika ya 36.

Zimbabwe sasa imefuzu mara tatu katika histori ya AFCON mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2004, 2006, 2017 na sasa 2019.

Imemaliza kundi la G kwa alama 11, mbele ya DRC ambayo imemaliza ya pili kwa alama 9.

Liberia ambayo ilienda Kinshasa na matumaini makubwa ya kufuzu, imemaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 7 huku Congo Brazaville ikiwa ya mwisho kwa alama tano.

More in African Football